Thursday, 27 March 2014

MKWE WA OSAMA BIN LADEN ATIWA HATIANI KWA SHAMBULIZI LA KIGAIDI

Mkwe wa Osama Bin Laden, Suleyman  Abu Ghaith ametiwa hatiani huko New York kwa kula njama ya kuwaua wamarekani kwa kufanya kazi kama msemaji wa Al-Qaida baada ya mashambulizi ya septemba 11.

Mshatakiwa huyo mweny umri wa miaka 48 amesomewa mashtaka ya kuwaua wamarekani, kula njama ya kusaidia Al-Qaida na kuliunga mkono kundi la Al-Qaida. Mashtaka hayo yanaweza kumpelekea akafungwa jela maisha.

Abu Ghaith amekanusha mashtaka hayo kwa kudai hakuwahi kuwa mwanachama wa kundi la Al-Qaeda.

Abu Ghaith