Hukumu hiyo imelaaniwa na chama cha wanasheria nchini humo ambacho kimesema jeshi la Misri limerudisha udikteta ulioangushwa na wananchi mwaka 2011.
Maandamano yamefanyika nje ya mahakama hiyo punde baada ya hukumu hiyo kutolewa.
Mahakama imesema wafuasi hao wa Ikhwan wamehusika na mauaji dhidi ya maafisa wa usalama pamoja na kutatiza amani na utulivu ndani ya nchi.
![]() |
| Wafuasi wa Morsi wakilia nje ya mahakama baada ya hukumu kutolewa |
