Filamu hiyo imepigwa marufuku katika nchi nyingi za kiislamu kutokana na filamu hiyo kuwa kinyume na maadili ya kiislamu. Nuhu عليه السلام ni mmoja wa manabii wa kiislamu.
Zainut tauhid Saadi ambaye ni mwanachama wa Bodi ya udhibiti wa Filamu nchini Indonesia alisema filamu hiyo inawaumiza waislamu na wakristo hivyo haifai kuruhusiwa kuoneshwa nchini kwao.
Nchi za Qatar, Bahrain na Falme za Kiarabu tayari zimeipiga marufuku filamu hiyo. Aidha wanazuoni wa Misri pia wametoa wito ipigwe marufuku nchini Misri.
Baadhi ya vikundi vya kikristo nchini Marekani vimelalamikia filamu hiyo kuwa inamuonesha Nabii Nuhu عليه السلام katika njia isiyokubalika.
Filamu hiyo ilianza kupigwa picha julai, 2012 na maeneo iliyoigiziwa ni ya Dyrhólaey, Fossvogur, Reynisfjara, New York na maeneo ya Southern Iceland.
Mwigizaji Russel Crowe ndiye aliyeigiza kama Nabii Nuhu عليه السلام. Filamu hiyo yenye dakika 139 inatarajiwa kuzinduliwa leo machi 28 na kuanza kuoneshwa Aprili 4 mwaka huu katika nchi mbalimbali duniani.
![]() |
| Russel Crowe katika filamu ya Noah |
