Wednesday, 26 February 2014

MUFTI WA GAZA SHEIKH ABDEL-KARIM AL-KAHLOUT AFARIKI DUNIA

mufti wa Gaza Sheikh Abdel-Karim al-Kahlout amefariki dunia usiku wa jumatatu katika Hospitali ya Shifa ya mjini Gaza akiwa umri wa miaka 78, wizara ya afya imetangaza jumanne.

Sheikh Abdel-Karim al-Kahlout alikuwa akiumwa kwa muda mrefu kabla ya kufariki kwake. Mazishi yake yamepangwa kufanyia jana jumanne.

Waziri mkuu wa Gaza ismail Haniyeh na wawakilishi wa taasisi mbalimbali za kiislamu walitarajiwa kuhudhuria mazishi yake.

Sheikh Abdel-Karim al-Kahlout aliteuliwa kuwa Mufti wa Gaza na kiongozi wa zamani wa Palestina Marehemu Yasser Arafat.

Kama Mufti, alikuwa na jukumu la kutoa maoni ya kisheria (fatwa) kulingana na tafsiri ya sheria ya Kiislamu katika utawala wa Palestina.

Sheikh Abdel-Karim al-Kahlout