Monday, 17 February 2014

JOHN KERRY ATEMBELEA MSIKITI WA ISTIQLAL WA JAKARTA, INDONESIA

Waziri wa mambo ya nje wa marekani John Kerry jana alitembelea msikiti mkubwa kusini mashariki mwa Asia wa masjid Istiqlal uliopo Jakarta, Indonesia kwa ajili ya kutoa heshima zake kwa jamii ya waislamu.

Baada ya kuvua viatu vyake nje ya msikiti, ndipo aliporuhusiwa kuingia na kutembea katika jengo kubwa la msikiti huo akiwa pamoja na imamu wa msikiti Kyai Al-Hajj Ali Mustafa Yaqub. 

Kerry aliwaambia waandishi wa habari kwamba msikiti huo ni moja ya sehemu za ajabu kuwahi kuziona. "Nimefurahi sana kuwa hapa na ninamshukuru Imamu Mkuu kwa kuniruhusu kuja hapa".

Serikali ya Rais Balack Obama inajaribu kukarabati mahusiano yake na ulimwengu wa kiislamu ambao uliharibika chini ya utawala uliotangulia tangu uvamizi wa Iraq 2003.

akiwasalimia kina mama wa kiislamu
akiwasalimia kina mama wa kiislamu
akimulekeza jambo Imamu Kyai al-Hajj Ali Mustafa Yaqub
baada ya kuvua viatu akiingia msikitini
ndani ya masjid  Istiqlal  na imamu Kyai al-Hajj Ali Mustafa Yaqub