Thursday, 3 August 2017

MSIKITI WA ZAMA ZA UTAWALA WA OTTOMAN WASHAMBULIWA KOSOVO

Msikiti wa zama za utawala wa Ottoman umeshambuliwa Pristina kwa kuandikwa maneno ya kashfa na kejeli.
Msikiti wa zama za utawala wa Dola ya Ottoman uliokarabatiwa na shirika la TİKA kutoka Uturuki umeshambuliwa kwa kuandikwa maneno ya kashfa na chuki dhidi ya uislamu.

Muungano wa waislamu Kosovo umetoa tangazo Jumatano ambalo lililaani vikali tukio hilo ambalo linaoneka kuwa la kibaguzi.

Maneno ya chuki dhidi ya jamii ya waturuki yalionekana katika mabango eneo la msikiti huo.

Uongozi katika msikiti huo unaomba mamlaka husika kufanya uchunguzi ni kuwakamata waliohusika na kitendo hicho.