Monday, 29 May 2017

PAUL POGBA AENDA MAKKAH KUFANYA IBADA YA UMRAH

Mchezaji ghali zaidi duniani, nyota wa Ufaransa na timu ya Manchester United Paul Pogba,24, amewasili nchini Saudi Arabia Jumamosi ya mwezi wa Ramadhani na kufanya
ibada ya Umrah.
Pogba amewasili Mji wa Makkah siku tatu tu baada ya kuisaidia timu yake ya Manchester United kutwaa kombe la Europa League kwa kuifunga timu ya AFC Ajax mabao 2-0
huko Stockholm, Denmark.

Pogba aliposti video katika akaunti yake ya Instagram akiwa na mizigo yake nje ya nyumbani kwake akiwaeleza wafuasi wake kwamba, "nipo njiani kuelekea kumshukuru Mungu kwa ajili ya msimu huu, Tutaonana Manchester baada ya ibada yangu".

Baadae alituma picha katika ukurasa wake wa Facebook akiwa katika mavazi ya Ihram wakati wa swala ya Tarawih na akiandika ujumbe Ramadhan Kareem na kusema "Sijawahi kuona kitu kizuri katika maisha yangu kama hiki"

Hii sio mara ya kwanza, alishawahi kufanya Hija.